Mganga Mkuu Hospitali ya Mji wa Tarime, na wengine wawili wasimamishwa kazi baada ya ambulance kukamatwa na mirungi. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mganga Mkuu Hospitali ya Mji wa Tarime, na wengine wawili wasimamishwa kazi baada ya ambulance kukamatwa na mirungi.

Na Frankius Cleophace, Tarime.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime  Bw. Elias Ntiruhungwa amewasimamisha kazi watumishi watatu akiwemo kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya gari la wagonjwa la hospitali hiyo kukamatwa likisafirisha  dawa za kulevya aina ya mirungi wilayani Bunda mkoani Mara mnamo Julai 11, Mwaka huu.
Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mganga Mkuu (DM) Dkt Innocent Kweka, Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Amir Kombo na katibu wa Hospitali Rwegasira Karugwa kutokana na uzembe waliofanya mpaka kitendo hicho kinafanyika.
“ Namsimamisha kazi DMO, Mganga Mfawidhi na Katibu wa hospitali kuanzia leo hadi tutakapomaliza uchunguzi wetu ambao umeanza kubaini kwa nini gari la wagojnwa lilitumika kusafirisha madawa ya kulevya. Kama watabainika hawana hatia watarudi kazini”alisema Mkurugenzi huyo.
Ntiruhungwa amesema hawezi kuvumilia kitendo hicho ambacho kimechafua jina la Hamashauri yake na nchi kwa ujumla na kwamba yeyote ambaye atabainika kuhusika katika tu... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More