MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

 NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA TIMU ya kitaifa ya kufuatilia na kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi wakiwemo wakulima, imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa miaka saba baina ya wakulima na wafugaji wa Kwala,wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kufanikiwa kuumaliza .
Mgogoro huo unabaki historia baada ya wafugaji wa bonde la mto Ruvu  ,Mwembe Ngozi kupewa agizo la kuondoka na kuhamia eneo la Waya,  ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Ruvu ili kuwaacha huru wakulima ambao walikuwa wakipata hasara kutokana na mazao yao kulishiwa mifugo.  
Mkurugenzi msaidizi wizara ya mifugo na uvuvi, ambae pia ni mwenyekiti wa timu hiyo, Dr. Martin Ruheta, aliwataka wafugaji hao akiwemo Sauti Mbili na Masanja Kidirgo ambao wana ng'ombe zaidi ya 500 waondoke kuanzia march 18 mwaka huu. Aliwaomba, wafugaji hao na wengine waondoke huku serikali ikiendelea kutafuta maeneo ya kudumu, kwa wale ambao mifugo haitoenea kwenye ranchi hiyo. 
"Timu hii ilianza kazi mwezi octoba mwaka jana, mkoa wa Kigoma, ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More