MGUNDA AJITETEA KUTOMPANGA ALI KIBA, ASEMA ANAFURAHISHWA NA ANAOWAPA NAFASI WANAFANYA VIZURI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MGUNDA AJITETEA KUTOMPANGA ALI KIBA, ASEMA ANAFURAHISHWA NA ANAOWAPA NAFASI WANAFANYA VIZURI

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KUMEKUWA na maswali mengi kwa mashabiki mbalimbali wa soka baada ya kuona mshambuliaji wa Coastal Union, Ali Kiba haonekani uwanjani akiichezea timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Bara tangu asajiliwe mwanzoni mwa msimu huu.
Wengi wamekuwa wakisubiri mechi kubwa ambazo ni Coastal Union dhidi ya Yanga au Simba wakiamini labda umaarufu wa mchezaji huyo utafanya mchezo uwe na morali kubwa kutokana na wingi wa mashabiki wa timu zote mbili ambao pia ni mashabiki wa mchezaji huyo.
Jana kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union ilicheza na Yanga lakini Ali Kiba hakucheza japokuwa alionekana uwanjani akipasha misuli moto na wachezaji wenzake.
Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda alipoulizwa sababu za Ali Kiba kutocheza, alisema wakati ukifika mchezaji huyo ataitumikia timu yake.

Juma Mgunda (kulia), kocha wa Coastal Union akiwa na wasaidizi wake

“Naomba hili niliweke wazi, Ali Kiba ni mchezaji wa Coastal Union,  amesajiliwa na ni mtumishi wa Coastal Union, ukifika wakati wa... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More