MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DK.MISANYA BINGI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MUHIMBILI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DK.MISANYA BINGI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MUHIMBILI

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
NI pigo!Ndivyo unavyoweza kuelezea taarifa za kufariki dunia kwa Mhadhiri wa  Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dk.Misanya Dismas Bingi.
Dk.Misanya ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji maarufu nchini  wa Radio One na ITV amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuz Blog Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbii Aminiel Aligaeshi amesema Dk.Misanya amefia MOI ila mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Muhimbili.

 Dk.Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.Alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili  baada ya kupata ugonjwa wa kupooza(stroke) na kupelekwa katika chumba cha Uangalizi maalum (ICU).
Kwa sasa msiba upo eneo la Makongo Juu jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea.Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea kuhusu msiba huo.
Pia Michuzi Blog inaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na msiba huo mzito... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More