MHAGAMA APONGEZA MIRADI KAMBI YA MLALE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MHAGAMA APONGEZA MIRADI KAMBI YA MLALE

NA MWANDISHI WETU:Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amepongeza kazi za uzalishaji mali katika kambi ya Mlale.
Aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi kwenye kambi hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyopo Mlale kwa lengo la kuzungumza na kuangalia miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kambini hapo.
Waziri Mhagama alisema kuwa dira ya taifa kufikia 2025 ni kuongeza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii kufikia hadhi ya uchumi wa pato la kati kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati hapa nchini inayolenga kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa.  
“Miradi hii iliyoanzishwa hapa imekuwa na tija kubwa kwa jamii iliyokaribu katika kufanikisha upatikanaji wa ajira kwa vijana na kukuza uchumi na maendeleo ya wanamlale na watanzania kwa ujumla” alisema Mhe. Mhagama
Aliongeza kuwa, mageuzi ya kikosi cha JKT Mlale 842 yamekuwa ni makubwa sana hususan katika kuunga mkono maagizo ya Mhe. Rais, Dkt. Jo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More