MHASIBU AIAMBIA MAHAKAMA MALINZI ALIIKOPESHA TFF DOLA ZA KIMAREKANI 41,000 NA SH. MILIONI 22 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MHASIBU AIAMBIA MAHAKAMA MALINZI ALIIKOPESHA TFF DOLA ZA KIMAREKANI 41,000 NA SH. MILIONI 22

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHAHIDI wa tisa katika kesi utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania, Sereck Mesack (68) amesema kwamba aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi aliwahi kuikopesha taasisi hiyo dola za Kimarekani 41,000 mwaka 2016.
Mesack, ambaye ni Mhasibu wa zamani wa TFF, amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo.
Mesack alisema pamoja na dola 41,000 Malinzi pia aliikopesha TFF Sh. Milioni 22, fedha ambazo zilitumika kulipia posho na gharama za kuipeleke timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys nchi za Rwanda na Kongo.

Mbele ya wakili Mwandamizi wa Serikali, Shadrack Kimaro aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Nikson Shayo, Mesack alisema Februari 9, 2016 kitabu cha kutolea risiti namba 00710-00750 kilionyesha Malinzi aliikopesha TFF Sh Milioni 10 na ri... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More