MHASIBU WA JIJI ARUSHA ATUHUMIWA KUTAFUNA MILIONI 85 KILA MWEZI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MHASIBU WA JIJI ARUSHA ATUHUMIWA KUTAFUNA MILIONI 85 KILA MWEZI

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amemtaka mhasibu wa jiji hilo, Charles Jacob kujisalimisha polisi kwa madai ya kutafuna Sh 85 milioni za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, 2019 katika mizani wa mazao ya chakula.


Amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh 3.3 milioni kwa mwezi badala ya Sh 88 milioni, kwamba Sh 85 milioni kila mwezi hazijulikani zinapokwenda.
Jacob, msimamizi wa mizani hiyo pamoja na wafanyakazi wake wawili, Thobias Julius na Agness Loishiye wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha.
Madeni amewaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi kati Mkoa wa Arusha.
Akizungumza leo Jumamosi Julai 20, 2019 Dk Madeni amesema kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.
“Nilifuatilia muda mrefu ukusanyaji wa mapato nikagundua kuna ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhasibu huyo ndio maana l... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More