MIAKA 19 BILA RAIS WA KWANZA WA NCHI MPENDA MICHEZO, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MIAKA 19 BILA RAIS WA KWANZA WA NCHI MPENDA MICHEZO, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KADI namba moja ya uanachama wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, inadaiwa alipewa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye leo anatimiza miaka 19 tangu kifo chake, Oktoba 14, mwaka 1999.
Wakati Mwalimu Nyerere anafariki dunia, mimi nilikuwa mwandishi mchanga sana- wakati huo nipo kampuni ya Habari Corporation Limited, chini ya wamiliki wake wa awali akina Jenerali Twaha Ulimwengu.
Aliyekuwa bosi wangu wakati huo, Kenny Manara, aliyekuwa Mhariri wa gazeti DIMBA alinipa kazi ya kwenda Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru ulipowekwa mwili wa marehemu kwa ajili ya kuagwa ili kuandika habari juu ya wanamichezo waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu na kuchukua maoni yao.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwasabahi wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars miaka ya 1970

Hakika nilijifunza mengi sana kupitia msiba huo kwa kusikia, kuambiwa na kujionea. Miongoni mwa niliyoambiwa ni kwamba, Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa ana kadi namba moja ya Yanga SC na... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More