Miaka 45 ijayo nusu ya ajira duniani zitachukuliwa na roboti, Wataanza kuandika vitabu, kufanya upasuaji na kuendesha malori - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Miaka 45 ijayo nusu ya ajira duniani zitachukuliwa na roboti, Wataanza kuandika vitabu, kufanya upasuaji na kuendesha malori

Roboti ni kifaa cha kielektroniki chenye uwezo wa kimakenika, kinachotumika kufanya yaliyo nje ya uwezo wa binadamu. Japo kifasihi roboti ni sawa na mtumwa.Asili ya jina roboti ni lugha ya Kicheki yenye maana ya “mfanyakazi”. Mnamo mwaka 1920 Mwandishi wa vitabu, Josef Čapek aliandika tamthilia inayosimulia hadithi za viumbe wanaotengenezwa kama wafanyakazi na kutumia jina la “labori” kwa lugha Kilatini, lakini baadae kaka yake alimshauri kutumia neno lenye maana hiyo hiyo ya Kicheki ikawa “Roboti”.


Roboti hutumia mitambo na programu maalumu kuiongoza. Roboti za siku hizi zinauwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea. Hazihitaji tena uongozwaji wa moja kwa moja mfano kwa kubonyeza kitufe au kutumia sauti.


Roboti yawezakuwa imeundwa aidha kwa chuma au mwili wa kawaida. Na baadaye kuwekewa akili bandia (Artificial Intelligence). Wengi tumezoea kuona zile za chuma kwenye filamu. Na hatujazoea kuona zenye muundo kama wa binadamu.


Kuna aina kuu 6 za Roboti nazo ni Roboti Sahili,... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More