MIAKA MITATU YA JPM IMEONGEZA ARI YA KUFANYA KAZI-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MIAKA MITATU YA JPM IMEONGEZA ARI YA KUFANYA KAZI-MAJALIWA

*Ameimarisha nidhamu, uadilifu kwenye utumishi wa umma

*Ameboresha miundombinu ya reli, barabara, nishati, elimu na afya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja, kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi.

Mafanikio mengine ni ununuzi wa meli katika ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria pamoja na kufufua Shirika la Ndege la Tanzania ili kuimarisha usafiri wa anga na kukuza sekta mtambuka zikiwemo za utalii, afya, kilimo na kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (SGR).

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novema 6, 2018.

Amesema mafanikio mengine yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli ni kuendesha vita dhidi ya rushwa na ufisadi kwenye taasisi za umma sambamba na kuanzisha Mahakama ya Maf... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More