MICHAEL WAMBURA AENDELEA KUSOTA RUMANDE, MAHAKAMA YAMWAMBIA HAINA UWEZO WA KUMFUTIA KESI, KUMPA DHAMANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MICHAEL WAMBURA AENDELEA KUSOTA RUMANDE, MAHAKAMA YAMWAMBIA HAINA UWEZO WA KUMFUTIA KESI, KUMPA DHAMANA


Na Karama Kenyunko globu ya Jamii.
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura (52), kuaendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kueleza kwamba haina mamlaka ya kumfutia kesi wala kumpa dhamana katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili.

Hatua hiyo imefikiwa leo Februari 14.2019 baada Mahakama kupitia Hakimu Mkazi, Mwandamizi Kelvin Mhina kutupilia mbali mapingamizi yaliyowasilisha na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Majura Magafu akisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya chochote katika kesi hiyo hadi hapo itakapopata kibali cha kusikiliza kesi hiyo kutoka kwa DPP.

Katika mapingamizi yao, Magafu aliiomba Mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo sababu katika mashitaka yote 17 yalilofunguliwa chini ya Sheria ya Uhujumu uchumi yalitakiwa yafunguliwe kama mashitaka ya kawaida ya jinai ambayo yanamruhusu mshitakiwa kujibu.

Pia alidai kuwa katika maudhui ya hati ya mashitaka hakuna hata kosa moja la uhujumu uchumi ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More