Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) yashika kasi jijini Dar es salaam - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) yashika kasi jijini Dar es salaam

Na Jeshi la Polisi. Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO)  imeendelea kupamba moto huku Tanzania ikiwa imepata medali ya dhahabu katika mbio za mita 5000,Fedha moja na Shaba tano katika mchezo wa Karate.Mwanariadha Fabian Nelson ndiye aliyefungua pazia kwa kuipatia Tanzania medali ya dhahabu baada ya kuwapita wenzake kutoka Kenya ambao walipata medali za fedha na Shaba.
Matumaini makubwa kwa Tanzania yapo katika mchezo wa kulenga shabaha, Judo,  Mpira wa Miguu na Riadha kwa upande wa mbio ndefu ambapo wanariadha wanaoshiriki michezo hiyo wameonyesha kiwango kikubwa.Nahodha wa timu ya kulenga Shabaha Tanzania Inspekta  Noel seng'ng'e, amesema mchezo huo umekuwa mzuri kwani wameweza kutoa wachezaji wengi wazuri katika kulenga shabaha na wanaimani ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mchezo huo.Kwa Upande wake Kocha wa Timu ya Mpira wa Miguu John Tamba amesema vijana wake wako vizuri na morali ipo juu hasa ukizingatia ushindi walioupata katika mchezo wa awali b... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More