MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAREJESHWA…ITAANZA JUNI MWAKANI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAREJESHWA…ITAANZA JUNI MWAKANI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana kurejesha michuano maarufu ya Kombe la Taifa. 
Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari imesema kwamba mashindano ya Taifa Cup yatafanyika kati ya Juni na Julai kuanzia mwakani 2019.
Pamoja na hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF imepitisha kuchezwa kwa mashindano ya Vijana U15 katika mtindo uliokuwa unatumika kwenye Copa Coca Cola wakati yale ya U17 yenyewe yatahusisha klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili kwa pamoja. 
Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) na Katibu wake, Wilfred Kidau (kushoto) 

Nayo mashindano ya Kombe la Shirikisho yataanzia katika ngazi ya mkoa ambapo kila mkoa utakuwa na bingwa wake.
Wakati huo huo: Rais wa TFF, Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Matagi Yasoda aliyefariki dunia juzi.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais wa TFF Ndugu Karia amesema mama Yasod... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More