MICHUZI TV: TEAM SAMATTA WAIPAPASA TEAM KIBA KWA 4-2 MBELE YA WAZIRI DKT MWAKYEMBE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MICHUZI TV: TEAM SAMATTA WAIPAPASA TEAM KIBA KWA 4-2 MBELE YA WAZIRI DKT MWAKYEMBE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.Mechi ya hisani baina ya marafiki wa Ali Kiba na marafiki wa Samatta imechezwa leo Jijini Dar es Salaam huku mamia ya wananchi wakijitokeza kwa wingi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.Mechi hiyo mahususi kwa ajili ya uchangiaji wa fedha zitakazotumika kukarabati miundo mbinu ya mashuleni iliweza kukutanisha wachezaji kutoka timu mbalimbali za ligi kuu na nje ya nchi.Mchezo huo uliomalizika kwa Marafiki wa Samatta kuondoka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Marafiki wa Ali kiba ulikuwa ni wa ushindani kwa kila upande wakitaka ushindi.Timu ya marafiki wa Ali Kiba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib akifunga goli la kwanza na la pili ila mpaka mapumziko timu ya marafiki wa Samatta waliweza kupata goli moja na matokeo kuwa 2-1.Katika kipindi cha pili,Marafiki wa Samatta waliingia kwa kasi na kupata goli la pili kwa mkwaju wa penati na Haruna Moshi Boba... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More