MIGOGORO YA ARDHI YAMRUDISHA WAZIRI LUGOLA MKOANI MOROGORO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MIGOGORO YA ARDHI YAMRUDISHA WAZIRI LUGOLA MKOANI MOROGORO

Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola anatarajia kuwasili kwa mara nyingine Mkoani Morogoro leo, kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imeibua mifarakano baina ya wananchi Mkoani humo.Waziri Lugola, wiki iliyopita alimaliza ziara yake Mkoani humo iliyokuwa na lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kuhusiana na utendaji kazi wa Taasisi za Wizara yake.Lugola katika ziara yake Mkoani humo, alifanya mikutano ya hadhara ambapo alikutana na migogoro mbalimbali lakini kero kubwa kati ya hizo ni kuhusiana na ardhi ambayo inapelekea wananchi kuwekeana chuki, kujeruhiana, kufikishana Polisi pamoja na kuuana.Kati ya Wilaya tatu alizozitembelea alipokuwa Mkoani humo, ni Morogoro, Mvomero na Kilosa, licha ya wananchi kutoa kero zao mbalimbali, mgogoro wa ardhi uliibuka kwa sehemu kubwa hasa katika Wilaya ya KIlosa.Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Waziri Lugola alisema alipokuwa Wilaya ya Kilosa, alikutana na mgogoro wa ardhi ambapo umeleta mgaw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More