MIILI ILIYOPATIKANA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE SASA YAFIKIA 224 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MIILI ILIYOPATIKANA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE SASA YAFIKIA 224

*Waziri asema uwezo wa kivuko ilikuwa kubeba watu 101 lakini siku ya tukio kilibeba watu 265
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema hadi sasa idadi ya miili ya watu waliokufa kutokana na kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere imefikia 224.
Pia amesema uwezo wa kivuko hicho ni kubeba watu 101 lakini kimebainika kuwa watu ambao walikuwa kwenye kivuko hicho walikuwa 265 ambayo ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kivuko hicho.
Waziri Kamwelwe amesema hayo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa maziko ya miili tisa ambayo imezikwa na Serikali kati ya miili 224 iliyopatikana baada ya tukio hilo.Amefafanua kati ya miili hiyo 224 ambayo imepatikana wanawake ni 126,wanaume 71.Pia watoto wa kike ni 17 na watoto wa kiume ni 10
Pia amesema miili ambayo imetambuliwa ni waliotambuliwa ni 219 na wote wamechukuliwa na ndugu na miili ambayo bado haijatambuliwa ni watu wanne ambao hao watazikwa na Serikali leo.Ameongeza kuna miili ya wat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More