MILIONI KUMI ZA TIGO JIGIFTISHE ZAENDA KWA MUOSHA MAGARI TABATA DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MILIONI KUMI ZA TIGO JIGIFTISHE ZAENDA KWA MUOSHA MAGARI TABATA DAR
Kitita cha shilingi milioni 10 cha mshindi wa kila wiki katika promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, kimenyakuliwa na Iyaka Seifu Muinga, anayefanya kazi ya kuosha magari Tabata jijini Dar es Salaam.Muinga anakuwa ni mshindi wa pili wa zawadi ya shilingi milioni 10 baada ya milioni kumi ya kwanza kuchukuliwa na David John Mmuni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Akipokea zawadi yake katika eneo analofanyia  kazi kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushangama, mshindi huyo alielezea furaha yake na ksema kuwa Tigo imemkomboa kwa kuwa amepata mtaj wa kufungua biashara.
‘Nimefurahi sana kuibuka na mtaji huu kutoka promosheni ya Jigiftishe. Nitatumia pesa hizi kufungua biashara, ila kusema kweli sina mpango wa kuacha kazi yangu ya sasa,” Iyaka alisema huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake waliomsindikiza jukwaani kupokea zawadi.
Akiongea  wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yahe, Bushangama aliwataka wateja kuen... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More