Mino Raiola anataka kumtumia Alexis Sanchez kumpeleka Pogba Barcelona - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mino Raiola anataka kumtumia Alexis Sanchez kumpeleka Pogba Barcelona

Hali si hali Old Traford, zikiwa zimebaki siku mbili tu yaani leo na kesho kwa United kuanza kampeni zao za ligi kuu Uingereza msimu wa 2018/2019 mhuni mmoja ameanza kuwachefua.


Ni Mino Raiola wakala wa Paul Pogba ambaye inaonekana ana nia ya kufanya jaribio mteja wake avae jezi za Beko (Barcelona) katika msimu ujao wa ligi barani Ulaya.


Raiola huyu huyu ikumbukwe ndiye ambaye alifanikisha dili la Paul Pogba kujiunga na United akitokea Juventus katik hia usajili ambao ulidaiwa kugubikwa na faulu nyingi ambazo alifanya Raiola.


Raiola ameanza chokochoko kwa kusema kwamba mteja wake hapaswi kupewa mshahara anaopewa kwa sasa na anatakiwa apewe £450,000 kwa wiki kama anavyopewa Alexis Sanchez.Ikumbukwe kwamba hii sio mara ya kwanza kwa Raiola kuwafanyia United tukio la namna hii kwani hata mara ya kwanza alimpeleka Pogba Juventus kwa style kama hii hii anayotaka kumuondolea.


Kwa aina ya kocha kama Mourinho asiyevumilia mihemko haijafahamika kama atakubali kuburuzwa na Raiola katika wakati... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More