MISRI WAPIGWA 1-0 NA BAFANA BAFANA NJE AFCON BAADA YA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MISRI WAPIGWA 1-0 NA BAFANA BAFANA NJE AFCON BAADA YA

WENYEJI, Misri wametupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ katika mchezo wa hatua ya 16 Bora usiku wa Jumamosi Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Shujaa wa Bafana Bafana ni nyota wa Orlando Pirates ya nyumbani, Afrika Kusini, Thembinkosi Lorch aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 85 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Lebo Mothiba wa Strasbourg ya Ufaransa baada ya shambulizi la haraka wakitoka kushambuliwa.
Mshambuliaji wa Liverpool na mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mohamed Salah alishindwa kuzuia machozi baada ya mchezo huo timu yake, Misri ikitolewa mapema mno baada ya kushinda mechi zote za Kundi A. 

Misri wameungana na wana fainali wenzao, Cameroon kuishia hatua hii katika AFCON ya mwaka huu baada ya Simba Wasiofungika nao kuchapwa 3-2 na Nigeria katika mchezo uliotangulia Jumamosi. Ikumbukwe Cameroon walitwaa taji la AFCON Februari 5, mwaka 2017 baada ya kuichapa Misri 2-1 katika fainali Uwanja wa l'Am... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More