MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)

Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii
Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) limeipa wenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika taifa la Misri kwa mwaka huu wa 2019 baada yakuishinda Afrika Kusini kwa kura zakuwania uandaaji wa Michuano hiyo.
Mashindano hayo yalikuwa yaandaliwe na taifa la Cameroon kwa mwaka huu, mwezi Novemba CAF iliipokonya maandalizi hayo kutokana na kuwa na maandalizi hafifu. Misri itakuwa na muda wa miezi 6 tu kufanya maandalizi kwa ajili ya ugeni wa Mataifa 24 yatakayoshiriki Michuano hiyo mwezi June.
Hata hivyo itakuwa ni mara ya Tano kwa Misri kuandaa Mashindano hayo tangu mara ya mwisho mwaka 2006 ilipoandaa Mashindano hayo."Napenda kuishukuru Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF) kwa kutuamini kuandaa Mashindano haya makubwa barani Afrika na naishukuru Serikali yetu kwa kuunga mkono suala hili,’ amesema Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Misri (EFA), Hany Abu Rida.
"Tuliandaa Mashindano haya 2006 ambapo ilitupa sana changa... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More