Mkandarasi Mradi wa umeme Mtera atakiwa kumaliza kazi Oktoba, 2019 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mkandarasi Mradi wa umeme Mtera atakiwa kumaliza kazi Oktoba, 2019

Teresia Mhagama na Hafsa OmarMkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mtera, ameagizwa kumaliza kazi hiyo ifikapo tarehe 4 Oktoba mwaka huu ili kuwezesha vijiji takribani 70 katika mkoa wa Iringa na Dodoma kupata umeme wa uhakika kwani sasa wanapata umeme wenye nguvu dogo.
Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani tarehe 10 Septemba, 2019 mara baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo hicho na kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi, kampuni ya SUNIR kutoka Iran.
“Mwaka 2017, Novemba tulimpa mkandarasi huyu kazi ambayo alipaswa kumaliza  ndani ya miezi 18 lakini hajafanya kazi vizuri na kazi zinazofanyika hapa haziendani na hatua ambayo ilibidi ifikiwe kwa sasa.” Alisema Dkt Kalemani.
Aidha, baada ya kufika kwenye eneo la mradi huo, Dkt Kalemani alikuta vibarua wanne tu wapo kazini na mkandarasi wa kampuni hiyo kutoka nchini Iran hakuwepo eneo la kazi, hivyo alimuagiza msimamizi wa mradi huo kutoka TANESCO kuhakikisha kuwa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More