MKEMIA MKUU WA SERIKALI AAHIDI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA ZA UCHUNGUZI WA KIMAABARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AAHIDI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA ZA UCHUNGUZI WA KIMAABARA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dk. John Magufuli, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanya chunguzi mbalimbali na kuwa miongoni mwa maabara bora za uchunguzi kwa nchi za Afrika Mashariki.
Dk.Mafumiko ameyasema hayo jijini Da es Salaam wakati anazungumza na maofisa uhusiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo pamoja na waandishi wa habari katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya inayoendeshwa chini ya uratibu wa Wizara ya Afya.
Dk. Mafumiko amesema kuwa taasisi hiyo imeongeza uwezo zaidi wa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa kuchukua muda mfupi kutokana na serikali kununua mitambo ya kisasa ya uchunguzi inayowezesha kufanya uchunguzi kwa muda mfupi na kutoa majibu kwa haraka ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.
Amesema katika utoaji huduma za uchunguzi kwa muda mfupi na kusaidia vyombo vingine vya Ser... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More