Mkoa wa Kagera wavutiwa na uwekezaji wa TADB - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mkoa wa Kagera wavutiwa na uwekezaji wa TADB

Na mwandishi wetuSerikali ya mkoa wa Kagera imepongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) kwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 31 katika sekta ya kilimo mkoani kagera hali inayoongeza tija ya uzalishaji katika kilimo mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine aliyekuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya kilimo inayopatiwa mkopo na benki hiyo.
Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa uwepo wa Benki ya Kilimo katika tasnia ya kahawa mkoani kagera imeweza kusaidia ulipaji wa malipo ya awali ya shilingi 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda kwa mkulima mdogo mkoani humo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema Benki ya Kilimo inaendelea kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara na kwa sasa benki inalenga katika kuhamasisha unywaji wa kahawa ili kuongeza soko la ndani kwa zao la kahawa.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More