Mkude awaomba Watanzania kwa hili ‘Sisi ni Tanzania, sisi ni Taifa Stars, kwa pamoja tuungane’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mkude awaomba Watanzania kwa hili ‘Sisi ni Tanzania, sisi ni Taifa Stars, kwa pamoja tuungane’

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas MKude ameungana na Watanzania katika kuhakikisha wanaisapoti timu ya taifa  ‘Taifa Stars’ ambayo inakibarua kizito cha kuibuka na pointi tatu muhimu dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ hii leo.Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Mkude ameandika kuwa kama Watanzania kwa pamoja tuungane kuwaombea wawakilishi wetu.


”Sisi ni Tanzania. Sisi ni Taifa Stars. Kwa pamoja, tuungane kuwaombea wawakilishi wetu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda,” ameandika Mkude.Stas ikiwa chini ya nahodha mahiri Mbwana Samatta itashuka dimbani hii leo majira ya saa 10 alasiri kuikabili timu ya taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019.


The post Mkude awaomba Watanzania kwa hili ‘Sisi ni Tanzania, sisi ni Taifa Stars, kwa pamoja tuungane’ appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More