MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AKABIDHIWA UENYEKITI KAMATI YA SEKTA NDOGO YA HALI YA HEWA NCHI ZA SADC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AKABIDHIWA UENYEKITI KAMATI YA SEKTA NDOGO YA HALI YA HEWA NCHI ZA SADC


 Na Ripota Wetu,Michuzi TV
WAKATI Rais Dkt  John  Magufuli akielekea kupokea Uenyekiti wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk.Agnes Kijazi amekabidhiwa Uenyekiti wa Kamati ndogo ya Sekta ya hali ya hewa ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Aidha Dk.Kijazi amechaguliwa bila kupingwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za SADC “SADC Meteorological Association of Southern Africa (SADC-MASA)” kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka huu wa 2019.  
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari nchini imeeleza kuwa Wilbert Timiza Muruke  ambaye amemwakilisha Dkt. Kijazi amekabidhiwa nafasi hizo katika mikutano ya SADC-SCOM na SADC-MASA iliyofanyika kwa kufuatana jijini Windhoek, Namibia kuanzia Agosti 5 hadi 9 Agosti, 2019.  Imefafanua kuwa  Kama ilivyo kawaida baada ya Rais Dkt. John Magufuli kukabidhiwa Uenyekiti w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More