MKURUGENZI MKUU NIDA ANZA KWA KUKAGUA SHUGHULI ZA USAJILI KWENYE OFISI ZA WILAYA; NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKURUGENZI MKUU NIDA ANZA KWA KUKAGUA SHUGHULI ZA USAJILI KWENYE OFISI ZA WILAYA; NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt. Anold Mathias Kihaule, ameenza kazi kwa kukagua utendaji wa ofisi za Usajili za Mkoa wa Dar-es-salaam ambapo pamoja na mambo mengine amezungumza na wananchi na kutembelea ofisi ya Serikali ya Mtaa ambako huduma ya utoaji wa fomu na ugawaji wa Vitambulisho zinaendelea.
Katika ziara hiyo Dkt. Kihaule aliyekuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Mamlaka hiyo; amepongeza kazi nzuri inayofanywa na wafanyakazi wa NIDA na kusisitiza watumishi kuzingatia utoaji wa huduma unaozingatia viwango ili kuweza kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa wananchi.
Aidha amewashukuru viongozi na Watendaji katika Serikali za Mitaa kwa kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanapata Vitambulisho vya Taifa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa.
Dkt. Anold Mathias Kihaule aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Mkurug... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More