MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.MKURUGENZI mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo, leo Novemba 23.2018 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.
Mshtakiwa Mwaipopo ambaye pia ni mhandisi wa madini amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Mutalemwa Kishenyi na Jackilline Nyantori. 
Mbali na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yako manne, Mwaipopo pia anashtakiwa na shtaka moja la kula njama, shtaka moja la kuongoza kutendeka kwa uhalifu, shtaka moja la kughushi, mashtaka mawili ya kukwepa kodi.
Mshtakiwa Mwaipopo anatarajiwa kuunganishwa na washtakiwa wenzake ambao ni Rais wa zamani wa migodi hiyo,  Deogratias Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo ambao ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More