MKUTANO WADAU WA MAENDELEO ,MAAFISA WA SERIKALI NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUTANO WADAU WA MAENDELEO ,MAAFISA WA SERIKALI NA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII-TASAF WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

Na. Estom Sanga-DSM 
Mkutano wa siku tano utakaojadili utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza jijini Dar es salaam baada ya kukamilika kwa ziara katika maeneo ya utekelezaji wa Mpango huo katika mkoa wa Mwanza na kisiwa cha Unguja. 
Mkutano huo unaowashirikisha Wadau wa Maendeleo wanaochangia utekelezaji wa Mpango huo,Maafisa wa Serikali kuu na baadhi ya halmashauri na Wafanyakazi wa TASAF hufanyika kila baada ya miezi sita kwa kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango na kuona mfanikio na changamoto za utekelezaji kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi. 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa iliyoko mbele ya Mfuko huo,Wataalamu, Wadau wa Maendeleo ni kuhakikisha kuwa maelekezo ya Serikali ya kuweka utaratibu mzuri wa kuwashirikisha walengwa katika kufanyakazi kupitia Mpango wa Ajira ya Muda unazingatiwa kwa ukamilifu. 
Bw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More