MKUU MPYA WA MKOA WA SONGWE BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AWASILI KITUONI , AAHIDI KUENDELEZA MAZURI YA GALLAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUU MPYA WA MKOA WA SONGWE BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AWASILI KITUONI , AAHIDI KUENDELEZA MAZURI YA GALLAWA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela amewasili katika ofisi yake mapema leo asubuhi kufuatia kuteuliwa kwake kuuongoza Mkoa wa Songwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli Julai 28, 2018.
Brigedia Jenerali Mwangela amepokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya nne za Mkoa wa Songwe, wakurugenzi wa halmashauri tano za Mkoa huu, wakuu wa idara pamoja na watumishi wote wa ofisi yake.
Mara baada ya mapokezi hayo Brigedia Jenerali Mwangela amepokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa katika kikao cha pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama.
Gallawa amesema kuwa anayo furaha kumkaribisha Brigedia Jenerali Mwangela na anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kumteua Brigedia Jenerali Mwangela, na kuwa wale waliokuwa wakifurahia kuondoka kwake wakijua sasa wataanza kufanya kazi ndivyo sivyo wajue wamepata kiongozi ambaye ni makini zaidi”.
Ameongeza kwa kuwataka watendaji na wanasiasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii wakiwa na lengo la kumkomboa mwananchi wa Songwe kutoka katika umasikini na kuongeza pato la mkoa na taifa.Naye Brigedia Jenerali Mwangela amemshukuru Gallawa kwa kuweka misingi mizuri ambayo imelenga kuuinua Mkoa wa Songwe kiuchumi na kuahidi kuwa atahakikisha mazuri yote atayaendeleza hasa pale alipoishia.Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akipokelewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisaini kitabu ofisini kwake mapema leo mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>


Source: Issa MichuziRead More