MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI

Na Stella Kalinga, SimiyuMkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.
Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa  .
“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe,  ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo
“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukul... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More