MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AHAMASISHA VIJANA KUPIMA UKIMWI ILI KUJITAMBUA MAPEMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AHAMASISHA VIJANA KUPIMA UKIMWI ILI KUJITAMBUA MAPEMA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WANANCHI wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameelezwa kuwa wana kila sababu za kuhakikisha wanakuwa na afya bora na salama, kwani afya ni muhimu na afya ni mtaji mkubwa katika maisha ya binadamu.
Pia wamehimizwa kupima afya zao kwa lengo la kutambua iwapo wamepatwa na maambukizi ya UKIMWI au laa, kwani kwa atakaepatwa na ugonjwa huo ataanza kutumia dawa ya ARV  na hivyo ataishi maisha marefu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo wakati akizungumza na wananchi kuhusu kampeni inayoendelea ya  kupambana  na UKIMWI na kujenga jamii yenye uelewa na furaha.Kizigo amesema mbele ya wananchi kuwa Serikali ilianzisha kampeni ya Furaha Yangu iliyozinduliwa kitaifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Agosti  31 mwaka huu 2018
"Wilaya ya Namtumbo tumeendelea na kampeni hii ikiwa na lengo kuu la kuongeza kiwango cha u... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More