MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AONGOZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI NDANI YA HIFADHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO SOPHIA KIZIGO AONGOZA OPERESHENI YA KUONDOA WAVAMIZI NDANI YA HIFADHI

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Ulinzi na Usalama ikongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo imeamua kufanya operesheni maalumu ya kusaka na kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi ya Mbarang'andu ambapo kuna watu kadhaa wamekamatwa na sasa wanaohojiwa.

Akizungumzia operesheni hiyo Mkuu wa Wilaya Kizigo ameiambia leo, Michuzi Blog kuwa wameanza kuifanya juzi na jana (Desemba 4 na Desemba 5 mwaka 2018) ambapo mbali ya kamati ya ulinzi na usalama pia kulikuwepo na vikosi kazi na timu ya wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya hiyo na kwamba uamuzi huo wa kufanya msako umekuja baada ya doria ya kwanza iliyofanyika kwa njia ya anga (ndege) ambapo walijionea uharibifu uliofanyika kwenye hifadhi ya Ushoroba wa Selous , Niassa, Mbarang'andu , Kisungule na Kimbanda.

"Kwa kutumia usafiri wa anga ambao tumefanya kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi tumejionea namna ambavyo kuna uharibu wa mazingira.Hivyo jana tumeamua kufanya msako maalumu w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More