MKUU WA WILAYA UBUNGO AUPONGEZA UONGOZI WA DAWASA KWA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MKUU WA WILAYA UBUNGO AUPONGEZA UONGOZI WA DAWASA KWA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma ya maji safi na salama na kutoa zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri.
Hayo aliyasema wakati wa kikao kazi mkoa wa Ubungo kilichoandaliwa na Ofisi ya kihuduma Dawasa Mkoa wa Ubungo .
Akizungumzia utoaji wa huduma ya maji, Amesema kwa upande wa Wilaya ya Ubungo malalamiko ya maji yamepungua kwa asilimia kubwa tofauti na hapo awali.
“Napongeza uongozi wa DAWASA Ubungo kwa kuweza kusimamia mchakato mzima wa kutoa huduma ya maji hata wakati naenda kuzindua baadhi ya miradi ya maji kwenye Wilaya hii wananchi walikua na shamra shamra kubwa baada ya kukaa muda mrefu bila maji”
Amesema Makori , “katika Wilaya iliyokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ni hii ya Ubungo na kipindi nateuliwa kuja kuwa Mkuu wa Wilaya nilikuwa napokea malalamiko ya maji kila siku, ila kwa sasa idara ambayo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More