Mloganzila yapatiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mloganzila yapatiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 15 ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.Vifaa hivyo Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac Therapy System vimetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama Prof. Sang Lyun Nam akiwa na Daktari Bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu Prof. Seung -Kon Huh kutoka Korea Kusini. Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amesema vifaa hivyo vitasaidia utendaji kazi katika vyumba vya upasuaji, na kuongeza kuwa watalaam hao mbali na kutoa vifaa hivyo lakini pia wanafanya kazi na watalaam wa Hospitali ya Mloganzila hatua ambayo inasaidia wataalam wa hospitali hiyo kupata ujuzi zaidi.“Wataalam hawa tupo nao hapa Mloganzila na wapo tayari kufundisha watanzania kufanya upasuaji ambao hatufanyi, hata msaada huu waliotupatia ni jitihada zao wenyewe, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More