MMILIKI WA MABASI YA PRINCES MURO AFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MMILIKI WA MABASI YA PRINCES MURO AFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.MFANYABIASHARA na mmiliki wa mabasi ya Princes Muro, Majid Abdallah maarufu kama Kimaro (51) leo Oktoba 23.2018  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la wizi na utakatishaji wa mafuta.
Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali, Esther Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa mshtakiwa ametenda makosa hayo kati ya Januari 2015 na Januari 2018 katika maeneo tofauti ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika shtaka la wizi imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa aliiba Lita 15950.3 za Mafuta aina ya Diesel na Lita 10925.22 za Mafuta aina ya Petrol mali ya mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Katika shtaka la utakatishaji, imedaiwa, siku hiyo katika sehemu tofauti tofauti za jiji la Dar es Salaam,mshtakiwa alitakatisha Lita hizo za Mafuta  kwa kuyauza  na kuyabadilisha kwa fedha huku akijua kuwa mafuta hayo ni zao la kosa la wizi naa alifanya hivyo kwa lengo la kupoteza uhalisia wa mafuta.
Hata hivyo, mshtakiwa ha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More