MMONYOKO WA MAADILI CHANZO CHA UKATILI NDANI YA FAMILIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MMONYOKO WA MAADILI CHANZO CHA UKATILI NDANI YA FAMILIA

Kwa kipindi cha Miezi tisa Julai 2018 hadi Machi 2019 Jumla ya Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa ikilinganishwa na mashauri 13382 ya mwaka 2017/18 hali ambayo ni sawa na ongezeko la 34% ya migogoro ya ndoa hapa Nchini.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu Mkurugenzi wa Watoto wa Wizara hiyo Mwajuma Magwiza aliitaja changamoto ya maadili ya mmomonyoko wa maadili kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa hapa Nchini.
Magwiza aliongeza kuwa Vitendo vya ukatili kwa watoto ndani ya familia vimekithiri huku wahausika wakubwa wa vitendo hivyo wakiwa wanafamilia hili likijionesha katika takwimu za Jeshi la polisi za mwaka 2017 zinaonesha kuwa Jumla ya matukio ya ukatili kwa watoto 13457 yameripotiwa na Jeshi la polisi.
Alivitaja vitendo hivyo kuhusisha ukatili wa kingono wenye matukio 3,583, mimba za utotoni 1,323 akiongeza kuwa taarifa jeshi hilo imeonesha matukio ya mikoa ya kipolisi yenye ukatili mkubwa kuwa ni kinondoni matukio 2,426, Dodom... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More