MNYAMA SIMBA AMCHINJA MWARABU MCHANA KWEUPEEEE TAIFA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MNYAMA SIMBA AMCHINJA MWARABU MCHANA KWEUPEEEE TAIFADar es Salaam,

Klabu ya soka ya Simba Sports ya jijini Dar es salaam leo imewashangaza watanzania pamoja na waafrika wengi waliokuwa wakiufuatilia mchezo wao wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya vigogo wa Misri AL-AHLY kwa kuwapa kichapo cha goli 1-0 huku wakiutawala mchezo na wakicheza kwa kujiamini sana. 
Simba ikisapotiwa na mmiliki wao MOHAMED DEWJI ambaye naye alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo, walipata bao lao moja na la ushindi kipindi cha pili kupitia straika wao makini wa kimataifa Meddy Kagere a.k.a MK14 katika dakika ya 65 ya mchezo. 
Kagere alifunga kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa mshambuliaji mwenzake JOHN BOCCO na kumuacha golikipa wa Al Ahly akiwalaumu mabeki wake kwa kumuacha Kagere peke yake ndani ya box. 
Haya ni matokeo mazuri kimataifa kwa klabu hiyo ambayo imekuwa ikipata matokeo mabaya iendapo ugenini kwa msimu huu ikiruhusu kufungwa magoli zaidi ya 10. Ushindi wa leo unawafanya Simba kubeba point 3 muhimu na... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More