MNZAVA: WAKULIMA,WAFUGAJI ONDOENI UBINAFSI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MNZAVA: WAKULIMA,WAFUGAJI ONDOENI UBINAFSIMBUNGE wa korogwe vijijini Mh Timotheo Mnzava amewataka wananchi jamii ya wafugaji na wakulima waishio katika kata ya Mkalamo na Magamba Kwalukonge kumaliza tofauti zao na kuachana na ugomvi baina yao na malumbano yasio na tija ili kuleta maendeleo ya kata zao na Korogwe na taifa kwa ujumla. 
Ameyazungumza hayo leo katika mikutano yake na wananchi hao alipotembelea katika kata hizo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukutana na wananchi ambapo lengo kuu ni kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo. 
Mnzava amezitaka jamii zote mbili za wafugaji na wakulima kuondoa ubinafsi katika mioyo yao na kwa pamoja wawe na upendo baina yao na kuishi kindugu ili kulinda amani ambayo ni tunu kwa taifa la Tanzania. 
“Natambua changamoto yetu ya Ardhi, na naamini hata siku moja hatuwezi kufuta mashamba yote, kwasababu uwekezaji pia tunauhitaji lakini uwekezaji wenye tija, lakini hata ikitokea siku moja mashamba yote tukapewa kama hatuna matumizi bora ya ardhi, kama ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More