MO Dewji ashusha maombi Yanga - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MO Dewji ashusha maombi Yanga

Mfanyabiashara maarufu Tanzania, Mohammed Dewji maarufu kama MO Dewji ameguswa na hali ya sintofahamu inayoendelea kunako klabu ya Yanga.


Mohammed Dewji

MO amesema kuwa kwa sasa anaiombea klabu hiyo kwa Mungu ili waweze kupita katika kipindi hiki kigumu ambapo anaamini kuwa kuimarika kwa timu hiyo kutapelekea timu imara ya Taifa Stars.


Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba, tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya,“ameandika MO Dewji kwenye ukurasa wake wa Twitter.


MO Dewji ambaye ni moja ya watu wenye hisa nyingi ndani ya klabu ya Simba, amesema hayo ikiwa ni miezi minne sasa tangu klabu ya Yanga iingie kwenye utikisiko wa kiuchumi na mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi, ambayo yamepelekea matokeo mabovu ya klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa.


 


The post MO Dewji ashusha maombi Yanga appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More