MO DEWJI KUIPELEKA SIMBA SC KAMBINI MAREKANI, AU URENO KUJIANDAA NA MSIMU UJAO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MO DEWJI KUIPELEKA SIMBA SC KAMBINI MAREKANI, AU URENO KUJIANDAA NA MSIMU UJAO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Bodi ya Simba SC, Mohammed ‘Mo’ Dewji amesema Simba SC itakwenda kuweka kambi Ureno au Marekani kujiandaa na msimu ujao ili iendeleze rekodi yake ya kufanya vizuri.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Dewji pamoja na kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia ameelezea mikakati ya msimu ujao.
“Tunaanza kupanga maandalizi ya msimu, mimi binafsi naongea na timu za Ulaya na Marekani... kuna rafiki yangu anamiliki DC United (Marekani) nimeongea naye watualike tukafanye maandalizi Marekani, kuna uwezekano wa kwenda Ureno, kwenye wiki mbili zijazo tutajua timu itakwenda wapi,” amesema Mo Dewji.

Mohammed ‘Mo’ Dewji ataipeleka Simba SC Ureno au Marekani kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao 

Dewji amewapongeza wachezaji kwa kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara ya pili mfululizo, kufuatia ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Singida United Uwanja wa Namfua.
"Niwapongeza na kuwa... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More