MO DEWJI UPDATES: MSAKO MKALI UNAENDELEA WAKATI WAZUNGU WAWILI WAKITAJWA KUHUSIKA NA UTEKAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MO DEWJI UPDATES: MSAKO MKALI UNAENDELEA WAKATI WAZUNGU WAWILI WAKITAJWA KUHUSIKA NA UTEKAJI

*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar wafanya msako mkali kuhakikisha anapatikana
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuna Wazungu wawili wanasakwa kwa kuhusika kuratibu mpango wa kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji 'Mo'.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kwamba katika tukio hilo kuna wazungu wawili wanahusika kuratibu tukio la kutekwa kwa Mo Dewj.
"Tupo hapa kwa ajili ya kufuatilia tukio hili la kutekwa kwa Mo.Taarifa za awali ambazo tumezipata zinaonesha kuna Wazungu wawili wamehusika kuratibu tukio la Mo kutekwa."Tumeanza kufuatilia na wananchi wasiwe na wasiwasi,kikubwa watupe taarifa nasi tutazifanyia kazi," amesema Kamanda Mambosasa akiwa eneo la Hoteli ya Collessium  eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako tukio la kutekwa Mo linadaiwa kutokea.

KAULI YA MAKONDAKwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema taarifa za kutekwa kw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More