Mobetto awapa kashikashi waandishi, aingia Red Carpet na baunsa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mobetto awapa kashikashi waandishi, aingia Red Carpet na baunsa

Mrembo Hamisa Mobetto ambaye alikuwa host wa Miss Tanzania 2018 aliingia Red Carpet akiwa na mabaunsa ili kujikinga na waandishi wa habari ambao walimkimbilia kwa wingi baada ya kuonekana anaingia ukumbini hapo. Hata hivyo hakuna mwandishi ambaye alipata fursa ya kuzungumza naye zaidi ya Clouds Media ambao walikuwa wadhamini wa show hiyo.Mobetto alikimbia kuongea na waandishi wa habari kwa kuhofia kuulizwa maswali ambayo alihisi yatamtoa kwenye mood kwani yeye ndio host wa sherehe nzima ya kumtafuta Miss Tanzania.


Siku kadhaa nyuma mrembo huyo alikumbwa na tetesi za kutaka kumloga baba wa mtoto wake Diamond Platnumz kwa madai ya kutaka gari pamoja na nyumba.


Shuhudi Mobetto alivyowakataa waandishi wa habari:-By Ally Juma


The post Mobetto awapa kashikashi waandishi, aingia Red Carpet na baunsa appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More