Mobetto kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza Miss Tanzania toka atuhumiwe kuroga na Diamond - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mobetto kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza Miss Tanzania toka atuhumiwe kuroga na Diamond

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ndiye atasimama shoo wa shindano la Miss Tanzania ambalo litafanyika usiku wa leo September 08, 2018.


Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mrembo huyo kuonekana mbele ya watu baada ya siku chache zilizopita mzazi mwenzake, Diamond Platnumz kumtuhumu kwamba anairoga familia yake.


Mrembo huyo hakuwahi kuzungumza chochote toka tuhuma hizo zitolewe juu yake ambapo alionekana akiendelea na shughuli zake.


Meneja wa biashara wa mrembo huyo, aitwae Beatrice Ndugu alifunguka kwamba tuhuma hizo kwa mteja wake haziwezi mwaribia biashara zake na kwanza ataendelea kufanya vizuri.


Usiku huyo wa Miss Tanzania utapambwa na waimbaji kama Barnaba Classic, Ruby pamoja na wasanii wengine huku shughuli hiyo ikidaiwa itahudhuriwa na watu wengi mashuhuri.


The post Mobetto kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza Miss Tanzania toka atuhumiwe kuroga na Diamond appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More