Modric kusaini mkataba mpya - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Modric kusaini mkataba mpya

Luka Modric kusaini mkataba mpya


Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia, Luka Modric, amebadili maamuzi yake ya kuondoka Madrid, na sasa atasalia katika miamba hiyo ya Hispania.


Kumekuwa na taarifa wiki kadhaa, kwamba kiungo huyo atamfata Cristiano Ronaldo katika ligi ya italia.


Klabu ya Intermillan ndio walioonyesha nia ya kupata saini ya kiungo huyo, ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kombe la dunia mwaka huu 2018, nchini Urusi na pia amelisaidia taifa lake kufika hatua ya fainali ya Kombe la Dunia, ambayo walifungwa na Ufaransa.


Raisi wa Real Madrid, Frolentino Perez, amemshawishi Modrid kubaki, na atampa mshahara ambao utamfanya awe mchezaji wa pili aliyelipwa zaidi katika klabu ya Real Madrid nyuma ya Gareth Bale ambaye ndo anaongoza katika orodha ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa Santiago Bernabeu.


Source: Shaffih DaudaRead More