MOI KUANZA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU ILIYOZIBA KWENYE UBONGO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MOI KUANZA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU ILIYOZIBA KWENYE UBONGO

Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr. Mohamed Mohamed akifungua kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu.
Mkurugenzi wa ubora na uhakiki wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt Mohamed Mohamed leo tarehe 5/11/2018 amefungua kongamano la tano kimataifa la mafunzo ya madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika ukumbi mpya wa Mikutano MOI ambapo mafunzo yanafanyika kwa siku tano, siku mbili za nadharia na siku tatu za mafunzo ya vitendo ambayo itahusisha upasuaji.
Dkt Mohamed amesema kongamano hili la tano limehudhuriwa na zaidi ya madaktari 100 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Malawi, Namibia na nchi nyingine za Afrika, ulaya, na marekani ambapo mafunzo yatatolewa na Madaktari bingwa 8 wazalendo kutoka MOI na wengine 15 kutoka Marekani na Ulaya. Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More