MOLINGA AFUNGA MABAO MAWILI NA KUINUSURU YANGA KUCHAPWA NA POLISI, YATOA SARE 3-3 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MOLINGA AFUNGA MABAO MAWILI NA KUINUSURU YANGA KUCHAPWA NA POLISI, YATOA SARE 3-3

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC imenusurika kupoteza mchezo wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare ya 3-3 na Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Mshambuliaji mpya, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga ‘Falcao’ ndiye aliyeinusuru Yanga na fedheha leo baada ya kufunga mabao mawili kipindi cha pili timu ikitoka nyuma kwa 3-1 na kupata sare ya 3-3.  
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Mwinyimkuu, alyesaidiwa na Makame Mdogo na Joseph Pombe, Yanga walitangulia kupata bao kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji mkongwe, Mrisho Khalfan Ngassa.


Mshambuliaji Ditram Nchimbi anayecheza kwa mkopo kutoka Azam FC akafunga mabao matatu mfululizo kuanzia dakika ya 29, 55 na 58 kuipa uongozi timu ya kocha Suleiman Matola katika mchezo wa ugenini.
Hata hivyo, Molinga aliye katika msimu wake wa kwanza akafunga kwa kchwa dakika ya 22 akimalizia krosi kutoka kulia na klwa shuti la mpira wa adha... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More