Morata hoi, Kante na Jorginho wang’ara - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Morata hoi, Kante na Jorginho wang’ara

Chelsea wamefanikiwa kuifunga klabu ya Huddersfield Town mabao 3-0 na kumpa Maurizio Sarri ushindi wa kwanza katika ligi kuu ya England akiwa na The Blues.


Chelsea wamepata uongozi kupitia N’Golo Kante baada ya shambulizi la kushutukiza pamoja na Jorginho kuongeza bao la pili.


Baadae Pedro dakika 10 kabla ya Sarri kuondoka uwanjani kifua wazi.


Baadhi ya wachezaji wamefanya vizuri na waliofanya vibaya


Waliofanya vizuri: N’Golo Kante


Ujio wa Jorginho, Maurizio Sarri na mfumo wa Sarrismo, utamfanya N’Golo Kante kubadilisshiwa majukumu tofauti na hapo awali.N’Golo Kanté ana mabao manne tu tokea. Aajiunge na ligi kuu England


2015/16: 37 Michezo, 1 goal

2016/17: 35 Michezo, 1 goal

2017/18: 34 Michezo, 1 goal

2018/19: 1 Michezo, 1 goal


Baada ya Antonio Rudiger aliokoa mpira kwenye eneo lake la hatari kabla ya Jorginho ya kuhamisha mpira kwa Pedro ambaye alimpasia Willian aliyepiga krosi kabla ya Kante kuzamisha mpira wavuni.


Chelsea wamebadilika sana kwa namna wanavyocheza. Kante amecheza dimba la juu na amecheza vizuri zaidi kuliko Bakayoko aliyezoeleka kucheza nafasi hiyo.


Kante leo alicheza upande wa kulia akisaidia na Pedro na alicheza vizuri kama mchezaji amabye amekuwa akitumika nafasi hiyo. Sarri amekuwa na tabia ya kibadislisha wachezaj nafasi zao za uwaja na kufanya vyema pia.


Amefeli: Alvaro Morata


Huenda tatizo sio gundu la jezi wala nini. Alvaro Morata ndani ya Chelsea mambo yake sio mazuri kabisa. Anacheza kwa kujivuta kama Laudt. Maurizio Sarri bado anamwamini Morata ndio maana amekubali kuruhusu Michy Batshuayi kwenda kwa mkopo Valencia.

Upokeaji wake wa pasi ni mbovu, uwezo wake wa kutoa pasi ni mbovu, uwezo wake kuficha mpira umekuwa mdogo. Yaani anakosa kila kitu uwanjani.


Mwisho wa siku Sarri akwaruhusu Willian na Pedro kuingia wenyewe langoni na kujaribu kufunga kwa jitihada zao baada ya kuona Morata anayumba.


Amefaulu: Jorginho


Huko tunakoenda bila shaka baada ya Kante na Eden Hazard, basi Jorginho anaonhezeka kwenye kundi la wachezaji muhimu wa Chelsea.


Mwanzoni Jorginho alipotea baada ya viungo vya Hudders kujaa katikati. David Luiz akachukua uamuzi wa kucheza mipira mirefu kabla ya Jorginho kufanikiwa kumiliki dimba lake kisawasawa.


Jorginho amepoteza mipira minne tu kati ya 66 na kumfanya kuwa na wastani 93.9% zaidi ya mchezaji yeyote katika mchezo wa leo.


Amefeli: Ross Barkley


Ross Barkley hatuwezi kusema amecheza vibaya sana leo dhidi ya Huddersfield lakini hajafanya makubwa. Hajaonesha kwamba anahitaji nafasi kwa juhudi zote. Alicheza kawaida. Hajachangamka kabisa. Ametulia kana kwamba ni mchezani mwemye namba ya uhakika.


Matteo Kovacic yupo benchi na bola shaka akirudi ataongezeka dimba la kati pamoja a Kante na Jorginho hivyo hakuna nafasi kabisa kwa Barkley ambaye bado atapata ushindani mkubwa kutoka kwa Ruben Loftus-Cheek.


Amefanikiwa: Terence Kongolo


Dakika 30 za mwanzo Chelsea waliteseka sana kwa kwa Huddersfield iliyokuwa chini ya kamanda Terence Kongolo.


Kongolo amejiunga na Hudders kwa mkopo kabla ya kumchukua moja kwa moja.


Huyu mwanume kongolo amewashikilia haswa Morata, Pedro na Willian kwa muda na kuwafanya watafute mpira kwa tochi.


Chelsea FC imekuwa timu ya tatu kupata alama nyingi za ugenini.


925 @ManUtd

802 @ChelseaFC

800 @Arsenal


Source: Shaffih DaudaRead More