MOROGORO MARATHONI ILIVYOFANA BAADA YA KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA . - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MOROGORO MARATHONI ILIVYOFANA BAADA YA KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA .

Na Dixon Busagaga,Morogoro.
WANARIADHA Marko Joseph wa Singida na Amina Mohamed wa JKT –Arusha jana wamewek rekodi mpya baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wananume na wanawake katika mashindano ya Mbio mpya za Morogoro Marathon 2018.
Joseph alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kutumia saa 1:05:50 akifuatiwa na mwanariadha Faraja Lazaro w JKT –A rusha aliyemaliza mbio hizo zilizoanzia na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri akituia saa 1:0:04.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha mkongwe Dickson Marwa aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:07:42 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na mwanariadha Anthony Moya aliyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:07:42.
Kwa upande wa wanawake Amina Mohamed amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia saa 1:21:47 akifuatiwa n Rozalia Fabiani liyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:23:59 huku Monica Nicolaus akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2:00:08.
Washindi wa Mbio za Kilometa tano wametang... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More