Mpira umri, Fernando Torres kumalizia maisha ya soka nchini Japan (+Picha) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mpira umri, Fernando Torres kumalizia maisha ya soka nchini Japan (+Picha)

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid na Liverpool, Fernando Torres ameamua kwenda kumalizia maisha yake ya soka nchini Japan.Nyota huyo wa Hispania, Torres mwenye umri wa miaka 34 amethibitisha kutarajia kujiunga na klabu ya Sagan Tosu ya nchini Japan msimu ujao.Baada ya kuhusishwa na kutimkia Marekani au Australia hatimaye kupitia mkutano na waandishi wa habari leo siku ya Jumanne majira ya hasubuhi amethibitisha kuelekea bara la Asia ambapo atajiunga na rafiki yake Andres Iniesta nchini Japan.


Kuelekea kwake ligi ya Japan kunadhihirisha kuwa umri wake umekwenda na hivyo hawezi kucheza kwenye klabu zenye ushindani mkubwa na ndoto za kuyafikia mafanikio makubwa na hii wala siyo yeye wa kwanza wapo wakina Wayne Rooney, Andres Iniesta na wengine ambao wametimkia China kumalizia maisha yao ya soka.


The post Mpira umri, Fernando Torres kumalizia maisha ya soka nchini Japan (+Picha) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More