MRADI WA MAJI WA KIMBIJI NA MPERA UTASAIDIA UPATIKANAJI WA LITA MIL 260 KWA SIKU-PROF MBARAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MRADI WA MAJI WA KIMBIJI NA MPERA UTASAIDIA UPATIKANAJI WA LITA MIL 260 KWA SIKU-PROF MBARAWA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ametembelea mradi wa uchimbaji wa visima virefu vya Kimbijii na Mpera wenye thamani ya Bilioni 19.6  vitakavyosaidia kupatikana kwa lita za maji Milioni 260 kwa siku.
Mradi huo wa visima vya maji uliochini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) una lengo la kuongeza wingi wa maji katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kufikia lita Milioni 720 kwa siku kufikia mwaka 2032.
Prof Mbarawa akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA  Dkt Suphian Masasi ameweza kukagua visima hivyo na kuwataka wakandarasi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Akizungumza wakati wa kukagua visina hivyo, Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama na yatakayotosheleza kwa matumizi yao.
" Mradi huu wa Kimbiji na Mpera utakaotoa Lita Milioni 260 kwa siku utasaidia sana wananchi wa Dar es Salaam, ukichukul... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More